Vijana jazz


Vijana Jazz (pia wanajulikana kama Vijana Jazz Band au Vijana Jazz Orchestra) ni bendi ya muziki wa dansi ya Kitanzania. Bendi hiyo ilifikia upeo wa umaarufu wao katika miaka ya 1980. Vijana Jazz, kama bendi nyingi za dansi za nyakati hizo, ilifadhiliwa na taasisi ya serikali – Umoja wa Vijana. Umoja wa Vijana ulikuwa mrengo wa vijana wa chama tawala cha Tanzania – Tanganyika African National Union.[1] Wanamuziki mashuhuri ambao wamecheza katika Vijana Jazz ni Hamza Kalala, Hemedi Maneti, Issa Chikupele, na Manitu Musa.

  1. Askew, K. M. (2002). Performing the Nation: Swahili Music and Cultural Politics in Tanzania. Chicago: University of Chicago Press.

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search